Idadi ya vifo kwenye mafuriko na maporomoko ya udongo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeongezeka na kufikia karibu 400.
Hayo ni kwa mujibu wa kiongozi wa eneo la Kalehe Thomas Bakenga vilipo vijiji vilivyoathirika, ambapo amebainisha kuwa takriban miili 349 imepatikana baada ya mafuriko ya Alhamis.