Wachimba madini wafariki katika ajali ya moto katika mgodi wa dhahabu nchini Peru
2023-05-08 21:57:43| cri

Wachimba madini kadhaa wamefariki katika ajali ya moto iliyotokea jumamosi kwenye mgodi wa dhahabu kusini mwa Peru.

Vyombo vya habari nchini humo vimenukuu taarifa iliyotolewa na mamlaka ya mkoa wa Arequipa kuwa, karibu wachimbaji 27 wa madini wamefariki katika mgodi huo unaoendeshwa na kampuni ndogo ya madini mkoani humo.

Wahudumu wa afya na magari ya magonjwa yamepelekwa katika eneo la tukio ili kusaidia kutoa huduma za matibabu na uokoaji.