Rais wa China ampa pole mwenzake wa Rwanda kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa
2023-05-09 14:55:40| cri

Rais Xi Jinping wa China jana Mei 8 alimpa salamu za pole mwenzake wa Rwanda Bw. Paul Kagame kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa ambayo yamesababisha vifo na majeruhi na hasara za kiuchumi.

Rais Xi, kwa niaba ya serikali na watu wa China, ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na pole kwa majeruhi na waathirika wa maafa hayo nchini Rwanda, na kusema anaamini kuwa Wanyarwanda hakika wataweza kushinda changamoto na kujenga upya maskani yao.