Tanzania yapongezwa kuwa katika mwelekeo mzuri kwenye malengo ya Azimio la Malabo
2023-05-09 21:56:56| cri

Tanzania imetajwa kuwa mwelekeo mzuri wa kutekeleza ahadi zake chini ya Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP), unaojulikana kama malengo ya Malabo. Tanzania imepata alama za juu zaidi kuliko washirika wake wengine kwa kuweka mkazo katika kupunguza kwa nusu ya idadi ya watu maskini.

Alipowasilisha ripoti kuhusu utekelezaji wa malengo hayo miongoni mwa nchi saba za jumuiya ya Afrika Mashariki, mchumi mkuu wa kilimo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Bw. Furaha Marwa, amesema Tanzania na Rwanda zinaendelea kufanya vizuri katika utekelezaji, ikiwa ni pamoja na kuimarisha upatikanji wa fedha katika sekta ya kilimo, kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2025 na kupunguza umaskini kwa nusu ifikapo 2025.

Hatua nyingine ni pamoja na kukuza biashara ya ndani ya Afrika, kuhimili hatari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uwajibikaji wa pande zote na kujitolea kutimiza malengo ya CAADP yenyewe.