Rais wa China kuwa mwenyekiti wa mkutano wa kilele wa China na Asia ya Kati
2023-05-09 09:13:02| CRI

Mkutano wa wakuu wa China na nchi za Asia ya Kati utafanyika Mei 18 na 19 huko Xi'an, mkoani Shaanxi, na rais Xi Jinping wa China ataongoza mkutano huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema, mkutano huo utahudhuriwa na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Emomali Rahmon wa Tajikistan, Serdar Berdimuhamedov wa Turkmenistan na Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan.