Shirika la ndege la ATCL larejesha safari zake kati ya Dar- Guangzhou
2023-05-09 19:59:35| cri

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limerejesha safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou China kuanzia Mei 11, 2023, mara tatu kwa wiki kwa siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi kutokea Dar es Salaam (Tanzania) na Jumatano, Ijumaa na Jumapili kutokea Guangzhou (China).

Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amewataka abiria kutumia usafiri wa shirika hilo kwani ni rahisi na unatumia muda wa takribani saa kumi, na kuwafaa wanaokwenda kwenye shughuli za biashara, mafunzo au kikazi.

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian pia amesema kupitia ukurasa wake wa twitter amefurahishwa na kurejea kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania za kwenda na kurudi kati ya Dar es Salaam na Guangzhou, kwani litakuza biashara na utalii kupitia mabadilishano ya watu kati ya China na Tanzania.