Katibu mkuu wa UM alaani wizi wa vifaa vya WFP nchini Sudan
2023-05-09 09:21:31| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali uporaji uliotokea katika ofisi ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Naibu msemaji wa Katibu Mkuu huyo, Farhan Haq amesema, Guterres amesisitiza kuwa pande zote husika zinatakiwa kulinda na kuheshimu wafanyakazi na taasisi za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na hospitali, na kwamba inapaswa kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia ili kuokoa maisha.

Haq ameongeza kuwa, uporaji huo katika ofisi za WFP ni ukiukaji wa karibuni zaidi wa taasisi za kibinadamu tangu vurugu zilipotokea nchini Sudan.