China yataka mwanadiplomasia wa Canada aondoke kabla ya tarehe 13
2023-05-10 09:06:46| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imemtangaza mwanadiplomasia wa ubalozi mdogo wa Canada jijini Shanghai Jennifer Lalonde kama “mtu asiyekaribishwa” na kumtaka aondoke China kabla ya tarehe 13, Mei.

Akizungumzia uamuzi huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema hatua hiyo ni majibu ya uamuzi kama huo uliochukuliwa na Canada kwa madai yasiyo na msingi kwamba China inaingilia kati masuala ya ndani ya Canada. Amesema China kamwe haiingilii mambo ya ndani ya nchi nyingine, na madai hayo yasiyo na msingi yanalenga kuchafua sura ya China, na ni ghiliba za kisiasa.

Amesisitiza kuwa uamuzi usio na msingi wa Canada wa kumtangaza mwanadiplomasia wa China kama “mtu asiyekaribishwa” ni hatua mbaya ambayo inakiuka kanuni za msingi zinazoongoza uhusiano wa kimataifa, na pia ni pigo la makusudi kwa uhusiano kati ya China na Canada.