Watu 15 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza
2023-05-10 22:58:37| cri

Idara ya afya ya Ukanda wa Gaza Palestina, imesema watu 15 wameuawa na wengine 22 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza siku hiyo.

Idara hiyo pia imesema watoto wanne na wanawake watano ni miongoni mwa watu 15 waliofariki, na 7 kati ya 22 waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

Mapema tarehe 9 jeshi la Israel lilianzisha "Operesheni ya Ngao na Upanga" kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo mengi ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha hasara nyingi. Miongoni mwa waliofariki ni wanachama watatu waandamizi wa kundi la Jihad. Kundi hilo limetoa taarifa likisema upande wa Israel utalipa gharama kwa "uhalifu" wake.