Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema, China inatumaini kuwa suala la Abyei halitaathiriwa na mgogoro wa Sudan, na kuzitaka pande zinazohusika ziendelee kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya ufumbuzi wa suala la hadhi ya Abyei.
Balozi Dai Bing amesema Sudan na Sudan Kusini ni nchi zinazohusika na suala la Abyei, na suala hilo halitatatuliwa bila mazungumzo na ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Pia amesema China inapongeza juhudi za kikosi cha muda cha usalama cha Umoja wa Mataifa huko Abeyi katika kulinda amani na utulivu wa eneo hilo, na kwamba China itaendelea kutekeleza kithabiti jukumu la kulinda amani, na kuunga mkono kazi ya kikosi hicho, ili kuchangia usalama na utulivu wa eneo la Abyei.