Nchi za kusini mwa Afrika zakubaliana kutuma wanajeshi mashariki mwa DR Congo
2023-05-10 23:03:03| cri

Nchi za Kusini mwa Afrika zimekubali kutuma vikosi vyake kusaidia kutuliza ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako makundi yenye silaha yamekuwa yakiendelea kuwatesa raia kwa miongo kadhaa.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano maalum wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jumatatu, inasema jumuiya hiyo imeunga mkono kutumwa kwa kikosi cha kurejesha amani na usalama mashariki mwa DRC.

Uamuzi huo ulifikiwa kwenye mazungumzo yaliyohudhuriwa na wakuu kadhaa wa nchi wanachama wa SADC, akiwemo Rais Felix Tshisekedi wa DRC, mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na mawaziri nchi mbalimbali wanachama wa jumuiya hiyo.

Hata hivyo mkutano huo haukutaja idadi ya wanajeshi watakaotumwa, wala muda watakaotumwa nchini DRC.