China yaitaka Ujerumani iungane nayo kupinga Vita mpya ya Baridi
2023-05-10 09:08:20| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang ametoa wito kwa nchi hiyo na Ujerumani kuungana katika njia sahihi, kwa pamoja kupinga Vita mpya ya Baridi, na kutenganisha uchumi ama kuvunja minyororo ya ugavi, na badala yake, kuongeza uaminifu na nguvu katika amani na ustawi wa dunia.

Qin amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Berlin. Baerbock amesema, Ujerumani imeweka umuhimu mkubwa katika mawasiliano ya ngazi ya juu na ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali. Amesema ana matarajio mazuri kuhusu raundi ya saba ya mashauriano ya uongozi kati ya Ujerumani na China, ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza nje ya mtandao baada ya janga na virusi vya Corona, na ya kwanza kati ya serikali mpya za nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Qin Gang amesema, China na Ujerumani ni nchi kubwa zenye ushawishi duniani, na zinapaswa kuimarisha majadiliano na ushirikiano chini ya mazingira mapya ya kimataifa yanayokabiliwa na changamoto mbalimbali.