Mkuu wa misaada ya Umoja wa Mataifa awasifu wafanyakazi wa misaada wa Sudan na kuomba msaada wao
2023-05-11 10:00:40| CRI

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu, Martin Griffiths, amewapongeza wafanyakazi wa kibinadamu walio mstari wa mbele wanaotekeleza majukumu yao licha ya vurugu zinazoendelea nchini Sudan, wakati Umoja huo na washirika wake ukiongeza usambazaji wa misaada nchini humo.

Hayo yamesemwa jana na Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq. Amesema, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaongeza msaada wa dharura kwa watu milioni 4.9 katika miezi ijayo katika maeneo ambayo hali ya usalama inaruhusu.

Ameongeza kuwa, WFP inalenga kuzuia na kutibu utapiamlo mkali kwa watoto 600,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano pamoja na wamama wajawazito na wanaonyonyesha.