Rais wa China ampa salamu za pole mwenzake wa DRC kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa
2023-05-11 15:39:02| cri

Rais Xi Jinping wa China jana Mei 10 amempa salamu za pole mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa, ambayo imesababisha vifo na majeruhi kwa watu wengi na hasara kubwa za kiuchumi nchini humo.

Rais Xi, kwa niaba ya Serikali ya China na watu wake, ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na pole kwa majeruhi na waathirika wa maafa hayo. Amesema anaamini kuwa watu wa DRC hakika wataweza kushinda changamoto na kujenga upya maskani yao.