Ujumbe wa watu 40 kutoka China wafanya ziara nchini Tanzania kuangalia fursa za utalii na uwekezaji
2023-05-11 22:40:48| cri

Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amesema ujumbe wa watu 40 unaojumuisha wawakilishi wa kampuni za utalii za China na waandishi wa habari unatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kuangalia fursa mbalimbali za utalii na uwekezaji.

Balozi Kairuki amesema kwa ufadhili wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO) na Benki ya NMB, ujumbe huo umekuwa ukijumuisha mawakala wa usafiri, waandishi wa habari na watu wenye ushawishi kutoka China wanatembelea Tanzania kuanzia Mei 11 hadi Mei 23, chini ya uratibu wa ushirikiano na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar. Ujumbe huo unatarajiwa kutembelea Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam.

Wanahabari walio kwenye ujumbe huo unajumuisha wapiga picha kutoka vyombo vya habari vya China zikiwemo televisheni za mikoa ya Jiangsu na Guangdong inayoongoza kwa uchumi nchini China. Balozi Kairuki alisema ubalozi huo unatarajia kuvutia watalii wengi kutoka katika mikoa hiyo miwili na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuwaonesha vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.