Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema muungano wa taifa la China lazima utimizwe
2023-05-11 10:04:14| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amesema utaratibu wa kimataifa uliojengwa baada ya vita lazima ulindwe, na muungano wa taifa la China lazima utimizwe.

Qin ambaye yuko katika ziara ya siku tano katika nchi za Ujerumani, Ufaransa na Norway, alisema hayo jana mjini Berlin baada ya kutembelea eneo la kihistoria la Mkutano wa Potsdam. Amesisitiza kuwa 'Taiwan kujitenga na China' ni changamoto kwa haki na utaratibu wa kimataifa, na ni kinyume na mwelekeo wa historia. Amesema Azimio la Potsdam lililotolewa baada ya Mkutano huo limedhibitisha tena Azimio la Cairo linalosema kwamba ardhi ya China, ikiwa ni pamoja na Taiwan, inapaswa kurejeshwa China, na kuongeza kuwa hayo ni mafanikio makubwa ya Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti.

Amesema Marekani inadai kushikilia utaratibu wa kimataifa unaozingatia kanuni, lakini imepuuza Azimio la Potsdam lililoandaliwa nayo, na kuunga mkono na kufanya njama katika shughuli za kutafuta " Taiwan kujitenge na China," ili kuvuruga utaratibu wa kimataifa baada ya vita na kudhoofisha mamlaka na usalama wa China, hatua ambazo hazikubaliki kwa watu wa China.