Watu 6 wauawa kwenye shambulizi dhidi ya sinagogi nchini Tunisia
2023-05-11 21:39:38| cri

Shambulizi lililotokea usiku wa tarehe 9 karibu na sinagogi la kiyahudi kwenye Kisiwa cha Jarbah nchini Tunisia limesababisha vifo vya watu 6, ambao ni pamoja na walinzi watatu, watalii wawili na mshambuliaji.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia imesema mlinzi mmoja wa Kikosi cha ulinzi wa umma cha Tunisia aliwafyatulia risasi wenzake na kunyakua silaha, halafu akawafyatulia risasi walinzi wa doria karibu na sinagogi. Walinzi walimuua mshambuliaji huyo kwenye mapambano.