Benki ya Dunia imesema, utajiri mkubwa wa maliasili barani Afrika, ikiwemo madini, mafuta, gesi na metali za kipekee, kama ukitumiwa vizuri unaweza kuliinua bara hilo katika kiwango kipya cha ustawi, licha ya kuongeza kasi ya uhamaji wa kijani wa Afrika.
Katika ripoti yake iliyozinduliwa jana jijini Nairobi, Kenya, Benki hiyo imependekeza kuwa nchi za Afrika zinapaswa kutumia vizuri mahitaji yanayoibuka ya metali, hairdo kaboni na madini ya kipekee kufadhili miradi ya kijamii kama afya na elimi, kuinua uchumi wao na kuongeza upatikanaji wa nishati.
Ripoti hiyo imesema, serikali katika nchi za bara hilo zinaweza kuongeza mapato mara mbili zaidi kutokana na maliasili kwa kutunga sera na sheria endelevu, kutekeleza mageuzi, kuboresha utawala bora, na kuboresha usimamizi wa hazina za serikali.