Rais wa China afanya ukaguzi katika Eneo Jipya la Xiong’an
2023-05-11 10:11:34| CRI

Rais wa China, Xi Jinping, jana jumatano ametoa wito wa juhudi zaidi ili kuongeza uaminifu na kudumisha maamuzi, wakati nchi hiyo ikichukua hatua thabiti za kuendelea kupata maendeleo mapya katika kuendeleza Eneo Jipya la Xiong’an.

Rais Xi amesema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi katika eneo la Xiong’an, kaskazini mwa mkoa wa Hebei, na kuogoza mkutano wa kuboresha maendeleo ya eneo hilo.

Wakati wa ukaguzi huo, rais Xi alisema Xiong’an imeingia katika awamu ya kuendeleza ujenzi wa kiwango kikubwa na kwa wakati huohuo, kuchukua nafasi za kazi zisizo za muhimu kwa nafasi ya Beijing kama mji mkuu wa China.

Rais Xi pia alitembelea makazi ambayo watu zaidi ya 5,000 walihamishiwa, ambako aliongea na wafanyakazi wa eneo hilo na wakazi, na kueleza kuridhishwa na mazingira mazuri ya kuishi ya wakazi hao.