China yapinga madai ya Marekani ya ukusanyaji wa data za watu
2023-05-11 10:08:08| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amepinga madai yaliyotolewa na Marekani ya kukusanya data za watu, akisema madai hayo hayana msingi wowote.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken ameituhumu China kwa kukusanya data dhidi ya watu wa makabila madogo katika mikoa ya Xinjiang na Tibet, kama aina nyingine ya udhibiti na ufuatiliaji.

Wang Wenbin amesema, China ni nchi inayotawaliwa na sheria, na faragha za raia wote wa China, bila kujali makabila yao, zinalindwa kisheria.