Serikali ya Kenya kutumia dola milioni 731 kununua treni mpya ili kuiboresha reli ya SGR
2023-05-12 23:37:53| cri

Serikali ya Kenya imeongeza matumizi ya reli ya SGR ya Nairobi-Mombasa hadi kufikia dola milioni 731.53 za Marekani katika miaka mitatu ijayo ili kurekebisha reli hiyo, kujenga njia mpya za pembeni na kununua injini zaidi na mabehewa ya mizigo .

Ripoti kutoka Hazina ya Kitaifa ya Kenya inaonesha kuwa Wizara ya Uchukuzi ya nchi hiyo itapokea zaidi ya dola milioni 714 kwa ajili ya maendeleo ya reli hiyo kati ya Julai mwaka huu na Juni 2026.

Waziri wa miundombinu na Ujenzi wa Kenya Bw. Kipchumba Murkomen mwanzoni mwa mwaka huu alisema serikali ya Kenya Kwanza kwa ushirikiano na serikali ya China, wana nia ya kurefusha reli ya SGR kutoka Mai Mahiu, Naivasha hadi kwenye mpaka wa Uganda kupitia mpango wa miaka mitano ambao utawezesha njia ya reli ya mabilioni ya dola kutekelezwa kupitia Narok, Bomet, Nyamira, Kisumu, na Malaba.