Tanzania kushirikiana na China kwenye miradi uhifadhi mazingira
2023-05-12 22:38:23| cri

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Switbert Mkama amesema Tanzania inatarajia kupata miradi ya uhifadhi mazingira na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo nishati endelevu yenye thamani ya Sh trilioni 42.4, miradi ambayo itasaidia kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Amesema miradi hiyo itafadhiliwa na Benki ya Dunia, Taasisi ya Afrika 50 na Shirika la Nishati la Afrika kwa kushirikiana na kampuni ya China Renewable Energies.

Dk Mkama amesema fursa hiyo imekuja baada Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na marais wa Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Makamu wa Rais wa Angola na watendaji kutoka Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika, katika uzinduzi wa mtandao wa uzalishaji wa pamoja wa nishati endelevu kwa nchi za kusini mwa Afrika, na kujadili fursa za uwekezaji katika sekta hiyo na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.