Rais wa China ahimiza askari wa nyambizi wawe na uwezo wa juu
2023-05-12 10:02:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alijibu barua iliyoandikwa na askari wa kikosi cha nyambizi, akiwahimiza kuendelea kuongeza uwezo wao ili kukamilisha kazi na kujitahidi kuwa kikosi chenye uwezo mkubwa katika pande zote.

Rais Xi amesema, kikosi hicho kinachofanya kazi chini ya bahari kinabeba majukumu makubwa, na kuwataka watoe mchango zaidi katika kutimiza malengo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Umma la China itakapofika mwaka 2027.

Hivi karibuni, kikosi cha askari wa nyambizi walimwandikia barua rais Xi Jinping wakieleza dhamira yao ya kufanya mazoezi zaidi, kuimarisha maandalizi kwa ajili ya vita, na kuongeza uwezo wa ushindi kwenye vita. Kwenye barua yake, rais Xi aliwasifu kwa kubeba majukumu yao, kupata maendeleo mfululizo na kukamilisha kazi mbalimbali kwa mafanikio.