Rais Xi afanya ziara ya ukaguzi mjini Shijiazhuang, Hebei
2023-05-12 15:37:35| cri

Rais Xi Jinping wa China leo amefanya ziara ya ukaguzi huko Shijiazhuang, mji mkuu wa mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China.

Kwa nyakati tofauti rais Xi amekagua Taasisi ya Utafiti wa Kimsingi wa Teknolojia ya Kidijitali ya China, na Jumba la Maonesho ya Mipango ya Bustani ya Kimataifa ya Udaktari na Dawa za Kiviumbe la mji wa Shijiazhuang, ili kuelewa hali ya utafiti na uzalishaji katika mji huo.