Mtoto awe na moyo wa dhati wa kumshukuru mama yake
2023-05-14 11:58:30| cri

"Mama anashona nguo kwa ajili ya mtoto wake atakayefunga safari ndefu. Mtoto awe na moyo wa dhati wa kutaka kutoa shukurani kwa mama yake." Rais Xi Jinping wa China alisoma shairi hili mahiri la Enzi ya Tang wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China wa 2015.

Mwaka 1969, Xi Jinping ambaye wakati huo alikuwa hajafikia umri wa miaka 16, alikwenda kijiji cha Liang Jiahe mkoani Shaanxi. Kabla ya kufunga safari, mama yake Qi Xin alimshonea mfuko wa kuwekea sindano na nyuzi wenye maandishi ya “moyo wa mama”. Mfuko huo mdogo haukumbanduka Xi Jinping kwa miaka saba. Baada ya Xi Jinping kushika nafasi ya uongozi, Qi Xin alimwandikia barua na kumwambia awe na maadilifu na kujisimamia kwa nidhamu kali. Mafundisho hayo ya mama yake yaliweka msingi thabiti kwa Xi Jinping kuwa ofisa na mtu mwema.

"Familia ni darasa la kwanza kwa watu, na wazazi ndio walimu wa kwanza wa watoto.” Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi amesisitiza mara nyingi umuhimu wa ujenzi wa nidhamu ya familia.

Mwezi Desemba mwaka 2016, Rais Xi alipokutana na wawakilishi wa Awamu ya Kwanza ya Familia Bora ya China, alisisitiza kuwa inapaswa kurithisha maadili mazuri kwa watoto tangu utotoni mwao, kuwaongoza kuwa watu wema, kuwasaidia kuwa na moyo safi na kukua kwa afya njema, ili wakue na kuwa watu watakaotoa mchango kwa nchi na umma.

Wakati wa mwaka mpya wa 2017 aliwakumbusha wachina wote wasisahau upendo kwa familia kutokana na kazi kubwa.

Upendo wa mama unajenga mtindo wa familia ambao unaathiri nchi nzima. Hatua za maendeleo ya kila familia zinahimiza maendeleo ya nchi, na thamani zinazotolewa na kila familia zinachangia na kuwa msukumo wa ustawishaji wa taifa la China.