Wizara ya Afya ya Cameroon yasema kesi za surua zimeongezeka na kufikia 4,677
2023-05-15 21:45:31| cri

Wizara ya Afya ya Umma nchini Cameroon imesema, kesi za ugonjwa wa surua nchini humo zimeongezeka na kufikia 4,677, huku vifo 18 vinavyotokana na ugonjwa huo vikirekodiwa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, hali ya mlipuko wa ugonjwa wa Surua nchini humo inaleta wasiwasi mkubwa, na hii inatokana na idadi ndogo ya chanjo za ugonjwa huo zilizotolewa katika miaka ya karibuni, kuongezeka kwa idadi ya watoto ambao hawajapata chanjo.

Wizara hiyo imesema, ili kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo, kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya Surua na rubella itafanyika kuanzia June 28 hadi Julai 2.