Katibu mkuu wa UM atoa wito kwa Palestina na Israel kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita
2023-05-15 22:46:46| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliyofikiwa kati ya Israel na kundi la Jihad la Palestina.

Katika taarifa iliyotolewa jana, Guterres amesifu kazi muhimu ya upatanishi iliyofanywa na Misri, na kuzitaka pande zote zitekeleze makubaliano hayo kihalisi.

Katia taarifa hiyo, Guterres pia alitoa pole kufuatia vifo vilivyotokana na mapambano ya karibuni kati ya pande hizo, akieleza kuwa vita vinasababisha mateso yasiyo ya lazima kwa binadamu. Amesisitiza kuwa, utatuzi endelevu wa kisiasa unaofikiwa kupitia mazungumzo ndio unaweza kuleta amani ya kudumu, na kukomesha kabisa mzunguko wa vurugu hizo.