Serikali ya Rwanda imesema, watu 135 wamekufa na mmoja hajulikani alipo kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyotokea hivi karibuni katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Dharura ya nchi hiyo imesema, watu 110 walijeruhiwa katika majanga hayo, na watu wengine zaidi ya 20,000 wamekosa makazi baada ya nyumba 5,963 kubomoka katika mikoa mbalimbali nchini humo.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amerejea tena ahadi ya serikali yake ya kuwasaidia waathirika wa majanga hayo katika wilaya ya Rubavu nchini humo.