ATMIS yaongeza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi 2,000 mwezi Juni
2023-05-15 08:53:31| CRI

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema imeongeza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi 2,000 nchini Somalia ifikapo Juni.

Mohammed El-Amine Souef, mwakilishi maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU nchini Somalia na mkuu wa ATMIS, amesema kamati ya pamoja ya kiufundi yenye wajumbe kutoka kwa wadau wanaofaa, wakiwemo wa serikali ya Somalia, Ofisi ya Msaada ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, na ATMIS, wametambua na kukubaliana kambi za kijeshi zitakazokabidhiwa na ATMIS kwa Kikosi cha Usalama cha Somalia (SSF) au zivunjwe.

Souef ambaye alikuwa katika ziara rasmi ya kutembelea makao makuu ya Sekta ya 5 ya ATMIS huko Jowhar, alisema wakati ATMIS inapunguza idadi ya askari waliopo Somalia, SSF itaongeza idadi yake na kuchukua maeneo ambayo ATMIS itakabidhi.