Watu 33 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Burkina Faso
2023-05-15 08:54:16| CRI

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa watu wasiopungua 33 wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika eneo la Boucle du Mouhoun, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Gavana wa Mouhoun amesema kijiji cha Youlou kilikumbwa na shambulizi la kikatili, ambapo watu wenye silaha walishambulia raia waliojishughulisha na mambo ya kilimo cha mboga kwenye ukingo wa mto, na kusababisha vifo vya watu.

Tangu mwaka 2015, ukosefu wa usalama katika nchi hiyo umesababisha vifo vya watu wengi na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.