Idadi ya vifo vya wafuasi wa pasta Paul Mackenzie nchini Kenya yazidi 200
2023-05-15 14:21:55| CRI

Wapelelezi wa Kenya Jumamosi walifukua miili mingine 22 kutoka kwenye kaburi la wafuasi wa pasta Mackenzie katika mji wa pwani wa Kenya wa Malindi.

Akiongea na wanahabari, Kamishna wa Kanda ya Pwani Rhoda Onyancha alisema hadi sasa miili 201 imefukuliwa tangu kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki kwenye msitu wa Shakahola mwishoni mwa mwezi Aprili. Amesema idadi ya watu walioripotiwa kutoweka imeongezeka hadi 610, na kuongeza kuwa mshukiwa mmoja alikamatwa Jumamosi, na kuongeza idadi ya washukiwa kufikia 26.

Wapelelezi hao walisema wengi wa wahanga walikuwa watoto ambao waliambiwa na pasta Paul Mackenzie, kutokula wala kunywa ili "kukutana na Yesu." Mahakama imeruhusu ombi la polisi kutaka Mackenzie na mkewe wazuiliwe kwa siku 30.

Rais wa Kenya William Ruto ametaja tukio hilo kuwa la kigaidi.