UM watoa wito wa kuendelea na utekelezaji wa makubaliano ya kusafirisha bidhaa za kilimo kwa nje kupitia Bahari Nyeusi
2023-05-16 21:02:02| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa jana lilifanya mkutano juu ya hali ya kibinadamu nchini Ukraine, na kutoa wito wa kuendelea kutekeleza makubaliano ya usafirishaji wa bidhaa za kilimo kwa nje kupitia Bahari Nyeusi.

Katika taarifa yake, Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Martin Griffiths amesema, operesheni za msaada wa kibinadamu bado zinaendelea kufanyika chini ya mazingira hatarishi, na kutoa wito wa kutafuta utatuzi wa kusimamisha vita mara moja.

Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, China inaunga mkono utekelezaji wa makubaliano hayo na makubaliano ya uuzaji wa mbolea ya Russia kwa nje. Pia amesema, China inasisitiza tena kuwa inapaswa kulinda kithabiti usalama wa nyuklia, na kusimamia athari nyingine zinazoambatana na mapambano, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za kiutendaji, na kufanya juhudi za kuhimiza amani na mazungumzo.