Mkutano wa kilele wa ufumbuzi wa masuala duniani wa 2023 wafuatilia kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi
2023-05-16 19:02:48| cri

Mkutano wa kilele wa ufumbuzi wa masuala duniani wa 2023 umeanza jana jumatatu mjini Berlin, Ujerumani, ukiwa na kauli mbiu ya “Kuunda upya Jamii: Kuelekea Siku zijazo za Pamoja Zilizo Endelevu na Shirikishi ”.

Akihutubia mkutano huo wa siku mbili, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema, dunia yenye ncha nyingi inahitaji ushirikiano wa pande nyingi, na pande zote zinapaswa kutoa busara na kuhimiza utafiti wa teknolojia mpya kwa pamoja, ili kukabiliana na changamoto duniani, ikiwa ni pamoja na vita ya Russia na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi.

Aliyekuwa kaimu msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Susan Thornton, alipoongea na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) alisema, inahitajika kusikiliza sauti ya China na kuimarisha mawasiliano na China kwenye mkutano muhimu wa kimataifa kama huo, kitendo ambacho kinaweza kusaidia kutimiza ushirikiano zaidi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali duniani.