Kenya na Somalia jana zilikubaliana kufungua upya vituo vyao vya mpakani baada ya kufungwa kwa miaka 11.
Waziri wa Usalama wa Ndani na Uratibu wa Serikali ya kitaifa wa Kenya Bw. Kithure Kindiki amesema, kituo cha mpakani cha kaunti ya Mandera kitafunguliwa baada ya siku 30, na Liboi cha kaunti ya Garissa pamoja na Ras Kamboni cha kusini mwa Somalia vitafunguliwa upya baada ya siku 60 na siku 90 mtawalia.
Baada ya kufanya mazungumzo na waziri wa usalama wa ndani wa Somlia Bw. Mohamed Ahmed Sheikh Ali ambaye yuko ziarani nchini Kenya, Bw. Kindiki amesema, pande hizo mbili pia zinaangalia uwezekano wa kuongeza kituo cha nne cha mpakani cha kuingia Somalia.