Mapigano yameendelea kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, jumatatu wiki hii, huku sehemu za mashariki mwa mji huo zikishuhudia milipuko ya mabomu kutoka kwa jeshi la anga la nchi hiyo.
Katika taarifa yake, Jeshi la Sudan limesema, idadi kubwa ya silaha, risasi na mafuta zinazomilikiwa na kundi la waasi vimeharibiwa katika operesheni iliyolenga baadhi ya maeneo ya Sharq Al-Neel na maeneo yanayozunguka Hospitali ya Nile Mashariki.
Taarifa hiyo pia imesema, hakuna raia waliouawa katika operesheni hiyo, lakini kikosi cha RSF kimesema shambulio hilo limesababisha vifo na majeruhi kwa raia wasio na hatia, na uharibifu katika sehemu kubwa ya hospitali hiyo.