Mkutano wa kilele kati ya China na Asia ya Kati kuimarisha zaidi ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
2023-05-17 08:52:21| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema, mkutano wa kilele kati ya China na Asia ya Kati utafikia maoni mengi zaidi katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa sifa ya juu, na kuzihimiza pande hizo mbili ziendelee kuwa watangulizi wa ujenzi huo.

Bw. Wang amesema, rais Xi Jinping wa China amedumisha mawasiliano ya karibu pamoja na viongozi wa nchi tano za Asia ya Kati katika miaka 10 iliyopita, kuweka mpango wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa sifa ya juu, kufikia maoni muhimu ya pamoja kuhusu kuhimiza uunganishaji wa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na mikakati ya maendeleo ya nchi hizo tano, na kuonesha umuhimu wa kuongoza ujenzi huo.