China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada kwa nchi za Sahel
2023-05-17 08:53:12| cri

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, jana alitoa hotuba kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu suala la Sahel, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada unaokidhi mahitaji kwa nchi za eneo hilo.

Balozi Dai alisema, hivi karibuni, kutokana na hali ngumu na kali ya kimataifa na kieneo, nchi za eneo la Sahel zimefanya juhudi za kudumisha usalama wa pamoja, kurejesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa kikanda, na zimepata matokeo mazuri.

Balozi Dai pia alisema, kuhimiza maendeleo endelevu ni mwelekeo muhimu wa ushirikiano wa kivitendo kati ya China na nchi za ukanda wa Sahel. China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kutoa msaada zaidi kwa nchi za eneo hilo katika kupunguza umaskini, usalama wa chakula, uzalishaji wa kilimo na ufugaji, ujenzi wa miundombinu na ukusanyaji wa fedha wa maendeleo.