Kundi la kwanza la watalii kutoka China lawasili nchini Zimbabwe tangu China irejeshe usafiri wa nje
2023-05-17 23:27:00| cri

Kundi la kwanza la watalii kutoka China jana liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Victoria Falls nchini Zimbabwe, na kukaribishwa na wenyeji kwa ukarimu mkubwa.

Tangu China irejeshe usafiri wa nje kwa raia wake, soko la utalii duniani limeanza kurudi katika hali ya kawaida kutokana na kurejea kwa watalii wa China. Mamlaka za utalii katika nchi za Afrika kama Kenya, Afrika Kusini, na Tanzania, zimesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya watalii wa China kumeleta uhai kwa sekta hiyo, na kutarajia kuimarisha ushirikiano na China kwa kupanua sekta hiyo.