Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Sierra Leone wafanya mazungumzo
2023-05-17 08:57:13| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang amefanya mazungumzo na mwenzake wa Sierra Leone David J. Francis siku ya Jumanne mjini Beijing.

Qin Gang ameeleza kuwa huu ni mwaka wa kumi tangu rais Xi Jinping atoe sera yenye moyo wa dhati kwa Afrika, na kwamba pande hizo mbili zinatakiwa kutekeleza kwa pamoja makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, kuendelea kusaidiana, kukuza ushirikiano wenye ufanisi na kuimarisha uratibu katika mambo ya kikanda na ya kimataifa.

Kwa upande wake Francis ameisifu China kwa juhudi zake za kulinda amani na utulivu wa dunia, na kuunga mkono mapendekezo muhimu aliyoyatoa rais Xi Jinping, na kupenda kushirikiana na China katika kuhimiza kwa pamoja uhusiano wa kimatiafa kuwa kidemokrasia na kuifanya dunia iwe na ncha nyingi.

Aidha pande hizo mbili zimebadilishana maoni kuhusu hali ya Afrika na mageuzi ya Umoja wa Mataifa.