Rais Xi Jinping wa China ataka mkoa wa Shaanxi kufanya juhudi katika kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China
2023-05-18 21:22:57| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alisikiliza ripoti iliyotolewa na serikali ya mkoa wa Shaanxi na kamati ya CPC ya mkoa huo juu ya kazi zao ambapo ameutaka mkoa wa Shaanxi uwe na ujasiri na dhamira kujitokeza katika mstari wa mbele kwenye mchakato wa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China na kuwa mfano wa kuigwa katika eneo la magharibi mwa China.

Rais Xi ameuagiza mkoa huo kutoa kipaumbele katika kazi ya kutimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia hali ya jumla ya maendeleo ya nchi nzima na vilevile hali halisi ya mkoani humo, ili kupata mafanikio mapya katika nyanja mbalimbali kama vile kujitegemea na kujiendeleza katika sekta ya teknolojia, kujenga mfumo wa kisasa wa viwanda, kuhimiza maendeleo yaliyoratibiwa kati ya maeneo ya mijini na vijijini, kuinua kiwango cha kufungua mlango na kuimarisha uhifadhi wa mazingira n.k.