Mapigano bado yanaendelea nchini Sudan. Jana tarehe 17, mapigano yalitokea tena katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum. Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, mapigano hayo yameendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja na kusababisha zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo kuhitaji misaada ya kibinadamu.