Waziri wa Biashara wa Zambia Bw. Chipoka Mulenga amesema kuwa Zambia inatarajia kuvutia uwekezaji zaidi wa China katika Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika. Na kusisitiza kuwa Zambia haitakosa fursa inayotolewa na China kwa nchi za Afrika.
Bw. Mulenga alisema, Zambia inahitaji kujifunza uzoefu wa mafanikio wa maendeleo wa China na kutarajia kuanzisha uhusiano wa karibu wa kibiashara na China.
Habari zinasema, maonesho hayo yatafanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 2 mjini Changsha, China.