Umoja wa Mataifa wasema zaidi ya watu 80 wafariki kutokana na mafuriko nchini Ethiopia
2023-05-18 21:41:49| cri

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UNOCHA) imesema, zaidi ya watu 80 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya nchini Ethiopia.

Katika taarifa yake kuhusu hali ya Ethiopia iliyotolewa jumatatu, UNOCHA imesema mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa na watu kukosa makazi, na hivyo kuongeza mahitaji ya kibinadamu katika mikoa kadhaa nchini humo ikiwemo mkoa wa Somali, Oromia, na Afar.

Takwimu zilizotolewa na UNOCHA zinaonyesha kuwa mafuriko hayo yamesababisha familia zaidi ya 35,000 kukosa makazi, pia yamesababisha vifo vya watu 45, na zaidi ya mifugo 23,000 kufariki, huku ekari zaidi ya 99,000 za mashamba zikiharibiwa katika mkoa wa Somali pekee, ambao umeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.