Wakuu wa nchi tano za Asia ya Kati wawasili mjini Xi'an kuhudhuria mkutano wa kilele kati ya China na Asia ya Kati
2023-05-18 10:39:25| cri

 

Wakuu wa nchi tano za Asia ya Kati wamewasili mjini Xi’an, mkoani Shaanxi nchini China kuhudhuria mkutano wa kilele kati ya China na Asia ya Kati utakaofanyika kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 19 mwezi huu.

Viongozi hao ni rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, rais wa Tajikistan Emomali Rahmon, rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev na rais wa Turkmenistan Serdar Berdimuhamedov.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Xianyang mjini Xi’an, viongozi hao wamekaribishwa na wenyeji kwa ukarimu mkubwa.