WMO: Kuna uwezekano wa asilimia 66 wa halijoto duniani kuongezeka kwa nyuzijoto 1.5 katika miaka mitano ijayo
2023-05-18 22:40:03| cri

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) jana limetoa takwimu likisema kuwa, uwezekano wa halijoto duniani kuongezeka kwa nyuzijoto 1.5 katika miaka mitano ijayo umefikia asilimia 66.

Shirika hilo limesema, japo hali hiyo ya ni ya muda, lakini ni ishara ya kuharakishwa kwa mabadiliko ya tabianchi. Wanasayansi wanadhani ongezeko la nyuzijoto 1.5 ni kiwango muhimu cha ukomo, na likipita kiwango hicho, uwezekano wa kutokea kwa mafuriko, ukame, na moto wa porini utaongezeka kwa kiasi kikubwa.

Katibu mkuu wa WMO Bw. Petteri Taalas amesema, kuwa El Nino inatabiriwa kutokea katika miezi ijayo ambayo itaongeza sintofahamu kwa mabadiliko ya halijoto duniani na matayarisho yanahitajika kwenye nyanja zote ili kukabiliana na hali hiyo.