Marais wa China na Tajikistan wafanya mazungumzo
2023-05-18 14:43:29| cri

Rais Xi Jinping wa China leo huko Xi’an amefanya mazungumzo na mwenzake wa Tajikistan Emomali Rahmon aliyeko ziarani nchini China na kuhudhuria mkutano wa kilele kati ya China na Asia ya Kati.

Rais Xi amesema, tangu China na Tajikistan zianzishe uhusiano wa kibalozi, kutokana na juhudi za pamoja za pande mbili, uhusiano kati ya nchi mbili umepanda ngazi kutoka jirani wa kirafiki hadi wenzi wa kimkakati, na kutoka wenzi wa kimkakati mpaka wenzi wa kimkakati wa pande zote. Mwaka 2019, rais Xi alifanya ziara nchini Tajikistan na kutangaza kwa pamoja kuunda jumuiya ya maendeleo ya pamoja na jumuiya ya usalama wa pamoja. Katika miaka minne iliyopita, ujenzi wa jumuiya kati ya nchi mbili umepata maendeleo makubwa.

Rais Xi amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Tajikistan  umekuwa na historia ndefu, msingi thabiti wa kisiasa, ushirikiano katika pande nyingi na unaungwa mkono na watu wa nchi hizo. China inapenda kufanya juhudi pamoja na Tajikistan kuinua kiwango cha ushirikiano wa pande mbalimbali, kuhimiza kujenga jumuiya ya China na Tajikstan yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya ujirani mwema na urafiki, na kunufaika pamoja na ustawi, ili kusaidia maendeleo ya nchi hizo mbili.