WANAWAKE NA USAWA WA KIJINSIA
2023-05-19 08:00:06| CRI

Katika vipindi vyetu mara nyingi tumekuwa tukizungumzia haki za wanawake na jinsi ambavyo wanawake wanajitahidi kujikwamua kutoka katika mfumo dume ambao umekuwepo kwa karne kadhaa. Lakini licha ya juhudi hizo, bado kuna pengo kubwa katika kutafuta usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali, iwe ni makazini, kwenye biashara, elimu, huduma za afya na maeneo mengine.

Ni kweli kwamba mfumo dume umekuwa ni kipingamizi kikubwa kwa wanawake kutimiza ndoto zao, kwani mara nyingi wamekuwa wakisikia kauli kama vile “wewe ni mwanamke huwezi kufanya hivyo” ama “kazi hii haiwafai wanawake”, ingawa ni kweli kwamba kuna baadhi ya kazi ambazo wanawake hawawezi kufanya, lakini kuna zile ambazo awali ziliaminika kuwa ni za wanaume lakini wanawake wamekuwa wakizifanya tena kwa umakini wa hali ya juu. Hivyo basi, katika kipindi chetu cha Ukumbi wa Wanawake hii leo, tutaangazia suala la ukosefu wa usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali.