Uganda yapongeza ushirikiano na China katika sekta ya kilimo
2023-05-19 08:50:51| CRI

Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Uganda Bw. David Kasura Kyomukama, amepongeza ushirikiano wa pande tatu kati ya nchi yake, China na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) chini ya mfumo wa ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Akiongea baada ya kukutana na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Bw. Kyomukama amesema miradi mbalimbali ya kupunguza umaskini imetekelezwa vijijini Uganda kupitia awamu ya tatu ya Mradi wa Ushirikiano wa FAO-China-Uganda, kwenye kilimo cha mtama, mpunga, upatikanaji wa maziwa na shughuli za ufugaji wa samaki na kuku.

FAO, Uganda na China mapema mwaka huu zilizindua awamu ya tatu ya mradi wa Ushirikiano wa FAO-China-Uganda, wenye lengo la kuwafikia zaidi ya walengwa 9,600 katika wilaya 20.