China yafanikiwa kurusha setilaiti ya 56 ya mfumo wa uongozaji wa Beidou
2023-05-19 19:08:52| cri

China imefanikiwa kurusha setilaiti ya 56 ya mfumo wa uongozaji wa Beidou jumatano wiki hii, kutoka katika Kituo cha Kurushia Setilaiti cha Xichang.

Kwa sasa setilaiti hiyo inafuatiliwa na Kituo cha Usimamizi wa Setilaiti cha Xi’an baada ya kufanikiwa kuingia kwenye obiti yake, na setilaiti hiyo mpya itajiunga rasmi na mfumo wa Beidou tarehe 25.