Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu Bibi Soipan Tuya, amesema Kenya inatoa kipaumbele kwenye urejeshaji wa ardhioevu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa ukarabati wa ardhioevu wenye azma ya kuimarisha ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi nchini Kenya.
Akiongea kwenye mkutano mjini Nairobi kwenye mkutano wa urejeshaji wa ardhioevu Bibi Tuya amesema kuwepo kwa muda mrefu kwa kaboni katika ardhi oevu kunapunguza kiasi cha kaboni hewani, na hivyo kupunguza ongezeko la joto duniani.
Amesema Kenya itaiga mpango wenye mafanikio wa kurejesha ardhioevu wa Afrika Kusini, ambao umesaidia upatikanaji wa ajira 37,000 hasa kwa vijana na wanawake.